Wednesday, March 6, 2013

MKURUGENZI WA ELIMU MAALUM(WIZARA)ATEMBELEA KITENGO CHA ELIMU MAALUM MWAYA

Mr.B.Kulwa-Mkurugenzi wa elimu maalum(katikati)akiwa na walimu wa kitengo cha viziwi Mwaya alipo watembelea tarehe 13.02.2013,Pamoja na ziara hiyo aliambatana na wageni wa CBM-AUSTRALIA ambao ni marafiki wa maendeleo ya elimu kwa viziwi,Pamoja na kuangalia maendeleo ya ujenzi wa darasa la viziwi mkurugenzi alipata nafasi ya kuongea na walimu wa kitengo cha viziwi na wasioona na kutoa utaratibu wa ufundishaji wa  wanafunzi wasioona kwamba wanatakiwa wasome wakiwa kwenye darasa maalum bila kuwachanganya na wakawaida kuanzia darasa la kwanza mpaka la tatu.

Pia aliona upungufu mkubwa wa walimu wataalamu na kuagiza uongozi wa halmashauri ufanye utaratibu wa kuwahamishia walimu waliopitia mafunzo ya elimu maalum waliopo kwenye shule za kawaida wahamie Mwaya badala ya kuhamisha walimu wataalam waliopo kitengoni kwenda kwenye shule za kawaida,Aliongeza kuwa atafanya utaratibu wa kuwapanga walimu wengi zaidi Mwaya hivyo isitokee uongozi wa halmashauri  kuwachelewesha kwa makusudi kuwaleta Mwaya,Mwisho alisema Elimu maalum ni swala Mtambuka hivyo hatawavumilia wasimamizi wa elimu wanaopuuza elimu maalum kwasababu za maslahi binafsi badala ya kuwasaidia wanafunzi wenye ulemavu.

CBM WATEMBELEA KITENGO CHA VIZIWI MWAYA

Kitengo cha viziwi mwaya kilianzishwa tarehe 13.01.2009 na mwalimu Tumaini ngajilo(mtaalam wa viziwi).Mnamo mwezi Septemba 2009 kanisa la Anglikana dayosisi ya Ruaha walionyesha dhamira ya dhati ya kukisaidia kitengo hiki kwa kusaidia ujenzi wa madarasa kupitia mradi wa CBR unaofadhiriwa na CBM-AUSTRALIA. hapo ndipo mchakato ulipoanza wa kutafuta eneo litakalofaa kujenga madarasa ya viziwi.
Hapa ni wageni mbalimbali kutoka kanisa la Anglikana,CBM-AUSTRALIA,Mkurugenzi wa elimu maalum(wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi)ofisi ya elimu mkoa na wilaya,walimu na wajumbe wa kamati ta shule ambao walikuwa wakifanya tathmini ya maendeleo ya ujenzi huo tarehe 13.02.2013.

 Hapa wageni wa CBM wakiangalia darasa linalotumiwa na viziwi ambalo limegawanywa kwa ceiling board ili kupata madarasa matatu ndani ya chumba kimoja,kutoka kushoto,Mr.J.Katindasa(mwalimu mtaalam)Kirstin Lee Bostelmann(CBM-regional office of Kenya)Mr.T.Ngajilo(Mkuu wa kitengo cha viziwi),Simon Duffy(CBM-Australia).