Wednesday, March 6, 2013

MKURUGENZI WA ELIMU MAALUM(WIZARA)ATEMBELEA KITENGO CHA ELIMU MAALUM MWAYA

Mr.B.Kulwa-Mkurugenzi wa elimu maalum(katikati)akiwa na walimu wa kitengo cha viziwi Mwaya alipo watembelea tarehe 13.02.2013,Pamoja na ziara hiyo aliambatana na wageni wa CBM-AUSTRALIA ambao ni marafiki wa maendeleo ya elimu kwa viziwi,Pamoja na kuangalia maendeleo ya ujenzi wa darasa la viziwi mkurugenzi alipata nafasi ya kuongea na walimu wa kitengo cha viziwi na wasioona na kutoa utaratibu wa ufundishaji wa  wanafunzi wasioona kwamba wanatakiwa wasome wakiwa kwenye darasa maalum bila kuwachanganya na wakawaida kuanzia darasa la kwanza mpaka la tatu.

Pia aliona upungufu mkubwa wa walimu wataalamu na kuagiza uongozi wa halmashauri ufanye utaratibu wa kuwahamishia walimu waliopitia mafunzo ya elimu maalum waliopo kwenye shule za kawaida wahamie Mwaya badala ya kuhamisha walimu wataalam waliopo kitengoni kwenda kwenye shule za kawaida,Aliongeza kuwa atafanya utaratibu wa kuwapanga walimu wengi zaidi Mwaya hivyo isitokee uongozi wa halmashauri  kuwachelewesha kwa makusudi kuwaleta Mwaya,Mwisho alisema Elimu maalum ni swala Mtambuka hivyo hatawavumilia wasimamizi wa elimu wanaopuuza elimu maalum kwasababu za maslahi binafsi badala ya kuwasaidia wanafunzi wenye ulemavu.

No comments:

Post a Comment